Rapa Zex Bilangilangi amemtaka Gravity Omutujju kumuomba msamaha bosi firebase Bobi Wine la sivyo atafunza adabu kwa kumzushia kichapo cha mbwa msikitini.
Zex amesema alikerwa na kauli ya Omutujju kudai kuwa yeye ni mwanamuziki bora kutoka uganda kuwashinda wasanii wakongwe Bobi Wine, Jose Chameleone na Bebe Cool ambapo alienda mbali zaidi na kuwataka kustaafu muziki kwa kuwa muda wao umeshapitwa na wakati.
Msanii huyo amesema Omutujju anapaswa kuwaheshima kaka zake walioupambania muziki wa kizazi kipya kukubalika nchini uganda huku akimtaka ashindane kwanza na wasanii Weasel na Eddy Kenzo kabla ya kujilinganisha na Bobi wine.
“He needs to apologize or we’ll deal with him. Gravity should learn to respect elders. He needs to first deal with the likes of Weasel, and Eddy Kenzo before ranking himself with Bobi Wine,” Zex kwenye mahojiano yake hivi karibuni.
“I will meet him and teach him some discipline,” Ameongeza.
Utakumbuka Zex ni moja kati wasanii ambao walikuzwa kimuziki na Bobi Wine kupitia lebo yake ya Fire Base Entertainment na huwa hapendi kumuona mtu akimsema vibaya bosi wake huyo wa zamani.