You are currently viewing ZIARA YA ONE OF THEM ONES YAMNYIMA USINGIZI CHRIS BROWN

ZIARA YA ONE OF THEM ONES YAMNYIMA USINGIZI CHRIS BROWN

Staa wa muziki kutoka Marekani Chris Brown ana zaidi ya miaka 17 kwenye huu muziki, amefanya matamasha mengi katika kipindi cha miaka yote hiyo lakini bado haijamfanya kulizoea Jukwaa.

Breezy amefunguka kupitia Big Boy TV kwamba ziara yake ijayo pamoja na Lil Baby “One Of Them Ones” inamtia wasiwasi na kumnyima usingizi kabisa kwenye kuhakikisha anawapa furaha mashabiki ambao wamelipa pesa zao kuja kumtazama.

Ziara hiyo ya muziki ambayo itazunguka kwenye miji 27 ya Kaskazini mwa Marekani, itaanza Julai 15 mwaka huu

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke