Mwanamuziki wa Dancehall kutoka nchini Uganda Ziza Bafana ameachiliwa uhuru baada ya kukamatwa Februari 13 huko Kabale.
Bafana alikamatwa baada ya performace yake huko kabale nchini uganda huku sababu kubwa ya kukamatwa kwake ikitajwa kuwa alidinda kutumbuiza kwenye moja ya show huko kabale licha ya kulipwa pesa zote kabla ya ujio wa janga la korona, jambo lilowakasirisha waandaji wa show hiyo wakamtupa jela.
Inaelezwa kuwa bafana alitaka mapromota wa show hiyo wamuongezee pesa kabla kutumbuiza kutokana na show hiyo kuwa na idadi kubwa ya watu.
Baada ya msanii huyo kususia kutumbuiza, mashabiki walikasirishwa na kitendo hicho ambapo walizua vurugu na kuaharibu vitu vya thamani katika ukumbi wa kabale jambo lilowaacha mapromota wakikadiria hasara kubwa.
Hata hivyo inaripotiwa kuwa mapromota waliompelekea kukamatwa kwake walihamua aachiwe uhuru kwa masharti kwamba atatumbuiza kwenye show nyingine itakayoandaliwa na waandaji wa show hiyo.