Mwanamuziki anayesuasua kimuziki nchini Uganda Ziza Bafana hana furaha kabisa baada ya kutoonekana kwenye orodha ya wasanii wa kila mwaka ambayo hutolewa na msanii mwenzake Bebe Cool.
Bafana, ambaye alifanya vizuri mwaka wa 2021 kwa kuachia magoma makali anadai kuwa Bebe Cool alipoteza mweelekeo katika tasnia ya muziki nchini Uganda kwani siku hizi hajakuwa akiachia muziki mzuri kama kipindi cha nyuma.
Hitmaker huyo wa “Embuzi” amesema Bebe Cool,anatumia orodha yake ya kila mwaka ya wasanii waliofanya vizuri kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa kwenye vyombo vya habari nchini Uganda.
Ikumbukwe Bebe Cool hajawahi kuwa na uhusiano mzuri na mwanamuziki mwenzake Ziza Bafana baada ya msanii huyo kuanza kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya miaka kadhaa iliyopita.