Inaonekana misala haiishi kwa Ziza Bafana, baada ya msala wa kutupwa jela kwa kususia moja ya show yake wiki kadhaa zilizopita licha ya kulipwa pesa zote, Mwanamuziki huyo kutoka nchini Uganda ameingia tena kwenye headlines.
Hii ni baada ya kumshushia kichapo cha mbwa Deejay mmoja kwenye moja ya performance yake wikiendi hii iliyopita.
Ziza Bafana ambaye alikuwa ameshikisha performance yake na mzuka wa kutosha, alikasirishwa na kitendo cha deejay kucheza nyimbo zake zilizokuwa na sauti mbovu.
Msanii huyo alilazimika kusitisha kutoa burudani kwa mashabiki zake hadi pale Waandaaji wa onesho hilo walipomleta deejay mwingine ambaye aliweka mambo sawa.
Hata hivyo baada ya hali kutulia, Ziza Bafana alisikika akiwaelezea mashabiki zake kuwa madeejay wakati mwingine wanaudhi kiasi cha kuwafanya wasanii kutaka kuwapiga kutokana na ubovu wa sauti za mashine zao.