Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria Zlatan Ibile ameidondosha tracklist ya album yake mpya Resan.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amethibitisha hilo kwa kusema kuwa album yake hiyo ina jumla ya mikwaju 12 iliyowakutanisha wakali Barani Afrika kama Rayvanny , Davido , Sho Madjozi na wengine wengi.
Resan album inatarajiwa kuingia sokoni rasmi Novemba 5, mwaka 2021 na inaenda kuwa album ya pili kwa mtu mzima Zlatan Ibile baada ya zanku ya mwaka wa 2019.