You are currently viewing ZUCHU AKATAA DILI LA SHILLINGI MILLIONI 12 ZA KENYA KISA DINI

ZUCHU AKATAA DILI LA SHILLINGI MILLIONI 12 ZA KENYA KISA DINI

Msanii wa Bongofleva kutoka WCB Wasafi, Zuchu amekataa dili la kutangaza pombe lenye thamani ya Dola 108,000 sawa na shilling milllioni 12,468,600 za Kenya.

Kwa mujibu wa mtandao wa Africa Facts Zone, wameeleza Zuchu alikataa dili hilo kutokana na Dini yake, lakini pia ushauri aliyopewa na mama yake mzazi, Khadija Kopa.

“Tanzanian Singer, Zuchu rejected a $108,000 endorsement deal offer from an alcoholic brand to preserve her Islamic faith. Her mother, Tanzanian Music Legend, Khadija Kopa warned her against promoting such products earlier” mtandao huo umeeleza.

Utakumbuka hadi kufikia Julai mwaka 2021 Meneja wa WCB Wasafi, Sallam SK alieleza kuwa Zuchu anachukua zaidi ya milioni 3 za Kenya kwa ajili ya kufanya kazi ubalozi.

Zuchu alitangazwa kuwa chini ya lebo hiyo Aprili mwaka 2020 akiwa ni msanii wa pili ya kike baada ya Queen Darleen.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke