You are currently viewing ZUCHU ATAKA KUSHINDANISHWA NA WASANII WA KIUME

ZUCHU ATAKA KUSHINDANISHWA NA WASANII WA KIUME

Hitmaker wa “Sukari”, Msanii Zuchu amedai kwa uandishi wake kwenye muziki anafaa kuwekwa kwenye ligi ya wasanii wa kiume.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Zuchu amesema kupambanishwa na wanawake ni kuwaonea.

“Kwa uandiashi wangu yafaa kuwekwa kwenye ligi za wanaume, wadada wenzangu nitawaonea tu,” amesema Zuchu.

Kauli ya Zuchu inakuja kipindi anatarajia kuachia nyimbo mbili kwa pamoja.

Utakumbuka Zuchu kutoka WCB Wasafi kwa sasa anafanya vizuri na nyimbo zake mbili, Jaro pamoja na Fire na juzi kati alitajwa kuwania tuzo za AFRIMA 2022 kwenye kipengele cha msanii bora wa kike Afrika Mashariki akichuana vikali na wasanii wengine kutoka ukanda huu

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke