You are currently viewing ZUCHU ATAMBA KUWA MSANII WA KIKE ANAYELIPWA ZAIDI AFRIKA MASHARIKI

ZUCHU ATAMBA KUWA MSANII WA KIKE ANAYELIPWA ZAIDI AFRIKA MASHARIKI

Mwanamuziki nyota kutoka lebo ya WCB Zuchu ametamba kuwa ndiye msanii wa Kike ambaye alipwa zaidi Afrika Mashariki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zuchu ameandika tambo hizo huku Twitter akithibitisha kwamba ametoka kufunga dili kubwa zaidi siku ya jana.

“I am forever grateful for my fans, Y’all just made me the most paid female artist in East Africa, love ya’ll” .”Just closed one of the biggest deals today, alhamdulillah”. – ametweet Zuchu.

Hitmaker huyo wa ‘Sukari’, amedokeza pia ujio wa album yake mpya mwaka huu huku akiwataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kuipokea album hiyo.

“Promising you an album this Year, you deserved it get ready.”

Ikumbukwe Zuchu kwa sasa anafanya vizuri kupitia wimbo uitwao ‘Mtasubiri’ alioshirikishwa na bosi wake diamond platnumz, wimbo unaopatikana kwenye Extended Playlist (EP) mpya ya Diamond iitwayo FOA

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke