Msanii wa Bongofleva, Zuchu anatarajia kufanya ziara yake kimuziki (tour) nchini Marekani kuanzia Novemba 18 hadi Desemba 3 mwaka huu.
Ziara hiyo ya Zuchu ni pamoja na kutumbuiza kwenye hafla ya utoaji wa tuzo za African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) zitakazotolewa Novemba 19 huko Dallas, Texas nchini Marekani ambapo Zuchu anawania kipengele cha Msanii Bora Afrika.
Hii itakuwa ni ziara ya kwanza ya Zuchu nchini Marekani tangu ajiunge na WCB Wasafi Aprili mwaka 2020, hivyo anajiunga na Staa mwingine wa Bongofleva, Ali kiba ambaye tayari yupo nchini humo kwa ajili ya tour yake.