You are currently viewing Zuchu hana mpenzi wala mchumba -Khadija Kopa

Zuchu hana mpenzi wala mchumba -Khadija Kopa

Mama mzazi wa msanii Zuchu kutoka WCB Wasafi, Khadija Kopa amerejelea na kusisitiza kuwa mwanawe bado yuko singo na hana mwanaume yeyote awe mchumba au mpenzi.

Kopa amesema kutokana na umaarufu wa Zuchu, siku akipata mchumba dunia nzima itajua na itakuwa ni habari ya mijini na vijijini, ila kwa watu wawe na subira na kutopotoshwa na kile ambacho wamekuwa wakikisikia mitandoani na kwenye mablogu ya udaku.

“Zuchu bado yupo single, hana mpenzi wala Mchumba na wala hajanitambulisha kwa Mwanaume yoyote kwamba Mama huyu ndiye Mwanaume wangu, Zuchu ni maarufu hata mimi Mama yake ni maarufu siku atakapopata Mchumba akanitambulisha matajua tu muwe na subira,” alisema Khadija Kopa.

Ikumbukwe Zuchu anatajwa kuwa na mahusiano na Diamond Platnumz lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha hilo, ila mitandaoni wanaonekana kama wapenzi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke