You are currently viewing ZUCHU KULIPA MILLIONI 500 ZA KENYA KUONDOKA WCB

ZUCHU KULIPA MILLIONI 500 ZA KENYA KUONDOKA WCB

C.E.O wa WCB Wasafi, Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa Zuchu kuondoka katika Lebo hiyo atalipa takriban shilingi milllioni 500 za Kenya.

Kauli ya Diamond inakuja muda mfupi baada ya Babu Tale kutangaza Lebo hiyo itasaini wasanii wapya hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Babu Tale ameandika “Hivi karibuni tutasaini wasanii wawili kujiunga lebo ya Wasafi ila safari hii tumeamua msanii atakua na mashaidi wawili kutoka COSOTA na BASATA”

“Music ni biashara yetu na ni jukumu letu kukuza na kusimamia hii kazi, hatuwezi kuacha hata iwe vipi” amesema Tale.

Hadi sasa WCB iliyoanza kusaini wasanii tangu mwaka 2015, ina wasanii kama Diamond Platnumz, Queen Darleen, Lava Lava, Mbosso na Zuchu.

Utakumbuka WCB Wasafi haijasaini msanii mpya tangu Aprili 2020 walipomtangaza Zuchu ambaye alikuwa msanii wa pili wa Kike ndani ya lebo hiyo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke