You are currently viewing Zuchu kulipa millioni 9.6 kwa tuhuma za kuiba mashairi wimbo

Zuchu kulipa millioni 9.6 kwa tuhuma za kuiba mashairi wimbo

Mwimbaji wa Bongofleva kutoka WCB Wasafi, Zuchu huenda akakamuliwa millioni 9.6 kwa kudaiwa kuiba wimbo wa msanii wa Injili, Enock Jonas huku lebo yake ikionesha kutokuwa tayari kuzilipa fedha hizo.

Katika malalamiko hayo Jonas, amedai Zuchu amechukua sehemu ya kibwagizo na staili ya kucheza katika wimbo wake wa ‘Wema wa Mungu’ ambao ulitoka mwaka 2012 lakini ulijulikana zaidi kwa jina la ‘Zunguka’, akiutumia katika wimbo wake mpya ‘Kwikwi’.

Taarifa za madai hayo zilianza kusambaa mitandaoni kupitia barua iliyoandikwa na kampuni ya wanasheria ya Gerpat Solution, ambapo mmoja wake Gerlad Magubuka, ameiambia Mwananchi leo Jumamosi Oktoba 22 kuwa mteja wao alikwenda kuwalalamikia Zuchu kutumia kionjo cha wimbo wake huo.

Magabuka amesema tayari wameshawapelekea wahusika barua ya madai hayo na nakala nyingine wamepeleka Taasisi ya Hakimiliki Nchini (Cosota) na Shirikisho la Wanamuzi Tanzania (Shimuta).

Akizungumza na Mwananchi, Enock amesema amelazimika kuchukua hatua hiyo baada ya mazungumzo na upande wa Zuchu kushindikana kwa kumwambia kuwa katika madai hayo hata laki mbili hawawezi kumlipa.

Kwa upande wao Cosota kupitia Katibu Mtendaji wake, Doreen Sinare, amekiri suala hilo kutua mezani kwake na kueleza kilichofanyika ni wasanii wenyewe kuandikiana barua na wao wamepelekewa kama taarifa hivyo hawawezi kusema lolote kwa sasa wameacha wasanii wenyewe ndio wawasiliane kwanza na baadaye wao watakuja kuichambua na kuitolea tamko.

Kwa upande wake Babu Tale alipotafutwa kuhusiana na tuhuma hizo, alikiri kuwasiliana na msanii huyo na kumpa majibu hayo ya kutompa hela aliyoitaka.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke