Mwanamuziki kutoka nchini uganda Zulitums ametoa changamoto kwa wasanii nchini humo kuanza kutumia lugha ya kiingereza kwenye nyimbo zao ili muziki wa uganda uweze kufika mbali zaidi.
Zulitums amesema licha ya wasanii wa uganda kutoa muziki mzuri wengi wao wamekuwa wakitumia lugha ya luganda kwenye nyimbo zao jambo analosema limewafanya wasanii kushindwa kutanua wigo wa muziki wao kwenye nchini zingine.
Zulitums ni mmoja wa wasanii nchini uganda walioshindwa kuupeleka muziki wao kimataifa hadi pale alipojiunga na lebo ya muziki ya Black Avie iliyoko nchini Nigeria ambayo imebadilisha aina ya muziki wake.