You are currently viewing ZZERO SUFURI AFUNGUKA UKIMYA WAKE, ADOKEZA UJIO WA ALBUM YAKE MPYA

ZZERO SUFURI AFUNGUKA UKIMYA WAKE, ADOKEZA UJIO WA ALBUM YAKE MPYA

Msanii wa muziki wa gengetone Zzero Sufuri amefunguka sababu za ukimya wake kwenye muziki.

Akizungumza na Mungai Eve, Zzero Sufuri amesema alichukua mapumziko mafupi kwa ajili ya kujipanga vizuri kimuziki baada ya kuachia nyimbo kali.

Licha ya ukimya wake kwenye game ya muziki amesema amekuwa akifanyia kazi album yake mpya ambayo ingeingia sokoni mwezi juni mwaka huu ila kutokana na mambo yaliyo nje ya uwezo wake bado anaboresha baadhi ya nyimbo kwenye album hiyo ambayo itaachia rasmi ndani ya mwaka huu.

Mbali na hayo amekanusha madai yanayotembea mtandaoni kuwa wimbo wake wa “Zimenishika” hakufaidi na mirabi ya wimbo huo kwa kusema kwamba wimbo huo umefungulia milango mingi kwenye maisha yake ambayo hakudhani atawahi fanikisha.

Hata hivyo amenyosha maelezo kuhusu kuomba msaada mashabiki zake kwa kusema kwamba alichukua maamuzi hayo kwa ajili ya kuandaa video yenye ubora ya ngoma yake mpya iitwayo “Uptown Girl.”

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke